• HABARI MPYA

  Thursday, September 09, 2021

  ELIUD AMBOKILE AREJEA MBEYA CITY


  MSHAMBULIAJI Eliud David Ambokile amerejea rasmi Mbeya City baada ya misimu mitatu ya kucheza soka nje.
  Ambokile aliondoka Mbeya City mwaka 2019 kwenda TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambako baada ya msimu mmoja alihamia Nkana FC ya Zambia alikocheza pia kwa msimu mmoja kabla ya kurejea nyumbani.
  Ambokile aliibukia Mbeya City mwaka 2018 kabla ya kupelekwa Black Leopards ya Afrika Kusini alikocheza kwa nusu msimu kabla ya kurejea Mbeya City ambayo ilimuuza Mazembe msimu uliofuata.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ELIUD AMBOKILE AREJEA MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top