• HABARI MPYA

  Thursday, September 02, 2021

  RAIS SAMIA ATOA DOLA 100,000 CECAFA YA WANAWAKE

  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan ametoa dola za Kimarekani 100,000 kudhamini Klabu Bingwa ya Wanawake Afrika Mashariki na Kati mwaka huu.
  Hayo yamesema na Mwenyekiti wa Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Walllace John Karia leo Jijini Nairobi nchini Kenya ambako mashindano ya mwaka yanendelea nchini Kenya.
  Karia ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), amesema udhamini huo ni endelevu na kila mwaka Rais samia atakuwa dola 100,000 kwa ajili ya mashindano hayo ambayo kuanzia yatajulikana kama CECAFA Womens Samia Cup.


  Katika fedha hizo, bingwa ataibuka na kitita cha 30,000 USD, mshindi wa pili dola 20,000 wa tatu dola 10,000 na fedha nyingine zitatumika kwa mambo mengine katika mashindano hayo ikiwemo kutoa zawadi za wachezaji na marefa bora. 
  Kwa mwaka huu, Simba Queens ndio inaiwakilisha Tanzania huko na baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya PVP FC ya Burundi na sare ya 0-0 na Lady Doves WFC ya Uganda – watakamilisha mechi zao za Kundi A kwa kumenyana na FAD FC ya Djibouti kesho.
  Bingwa atashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye mwaka huu nchini Misri, ambayo itahusisha timu nane, nyingine kutoka kanda nyingine barani zitakazogawanywa katika makundi mawili.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS SAMIA ATOA DOLA 100,000 CECAFA YA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top