• HABARI MPYA

  Thursday, September 02, 2021

  RONALDO NDIYE MFALME WA MABAO DUNIANI


  MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo sasa ndiye mchezaji aliyeifungia mabao mengi zaidi kwenye mechi za kimataifa.
  Hiyo ni baada ya jana kufunga mabao mawili timu yake ya taifa, Ureno ikishinda 2-1 nyumbani dhidi ya Ireland kwenye mechi ya Kundi A kufuzu Kombe la Dunia.
  Sasa Ronaldo mwenye umri wa miaka 36, ambaye pia jana alikosa penalti iliyookolewa dakika ya 15, amefikisha mabao 110 katika mechi ya 180 za timu yake ya taifa.
  Mshambuliaji huyo wa Manchester United sasa amempiku mshambuliuaji wa zamani wa Bayern Munich na Hertha Berlin za Ujerumani, Ali Daei aliyefunga Iran mabao 109 katika mechi 149 kuanzia 1993 hadi 2006.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO NDIYE MFALME WA MABAO DUNIANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top