• HABARI MPYA

  Sunday, September 05, 2021

  MIRAJ MADENGE NA FAROUK SHIKARO WATUA KMC

   

  KLABU ya KMC ya Kinondoni Jijini Dar ea Salaam imeimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji kadhaa wazoefu akiwemo kipa Mkenya Faruk Shikaro na mshambuliaji mzawa, Miraj Athumani 'Madenge'.
  Shikaro aliidakia Yanga SC kwa misimu miwili iliyopita akotokea Bandari ya kwao, Mombasa wakati Miraj aliibukia timu ya vijana ya Simba mwaka 2013 kabla ya kwenda kucheza Toto Africans ya Mwanza 2015 hadi 2016 alipohamia Mwadui FC hadi 2018 alipojiunga na Lipuli kabla ya kurejeshwa Msimbazi mwaka 2019.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MIRAJ MADENGE NA FAROUK SHIKARO WATUA KMC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top