• HABARI MPYA

  Sunday, September 05, 2021

  ADAM ADAM AJIUNGA NA POLISI TANZANIA

   

  TIMU ya Polisi Tanzania imemsajili mshambuliaji chipukizi wa kimataifa nchini, Adam Omar Adam aliyevunja mkataba na klabu ya Al-Wahda ya Tripoli nchini Libya.
   Adam mwenye umri wa miaka 24, alijiunga na Al-Wahda ya Jijini Tripoli Juni mwaka jana kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka JKT Tanzania.
  Lakini pamoja na mwanzo mzuri, lakini ameshindwa kumalizia mkataba wake na anarejea nyumbani baada ya msimu mmoja tu wa kucheza Ligi Kuu ya Libya.
   ya usajili huo, Adam Adam alikuwa akiitumikia klabu ya JKT Tanzania na hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao Saba katika Ligi Al Wahda ilimsajili Adam baada ya kung'ara katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2019/2020 akifunga mabao 13.
  Tayari kikosi cha Polisi Tanzania yenye maskani yake mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kimeweka kambi mjini Mwanza kujiandaa na msimu wa tatu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara tangu ipande.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ADAM ADAM AJIUNGA NA POLISI TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top