• HABARI MPYA

  Wednesday, September 01, 2021

  AZAM YASAJILI BEKI MCAMEROON ALIKUWA ANACHEZA ZAMBIA

  KLABU ya Azam FC imemsajili wa beki wa kati Mcameroon, Yvan Lionnel Mballa, kwa mkataba wa mwaka mmoja kutoka Forest Rangers ya Zambia.
  Mballa anahitimisha zoezi letu la usajili kwenye dirisha hili, akikamilisha idadi ya wachezaji wapya nane tuliowasajili.
  Wengine wapya waliosajiliwa Azam FC iliyopo kambini Jijini Ndola nchini Zambia kujiandaa na msimu mpya ni viungo, Mkenya Kenneth Muguna, Wazambia Paul Katema, Charles Zulu na washambuliaji Rodgers Kola na Mkongo Idris Mbombo.
  Azam FC pia imesajili wazawa wawili wapya, kipa Ahmed Ali Suleiman 'Salula' kutoka KMKM ya Zanzibar na beki, Edward Charles Manyama kutoka Ruvu Shooting ya Pwani.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM YASAJILI BEKI MCAMEROON ALIKUWA ANACHEZA ZAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top