MABINGWA watetezi, Arsenal wamepangwa kucheza na timu ya Daraja la Kwanza, Burnley katika Raundi ya Nne ya Kombe la FA, England.
Washika Bunduki wa London ambao wanataka kushinda taji hilo maarufu kwa mwaka wa tatu mfululizo, waliifunga Sunderland 3-1 Jumamosi na kusonga mbele.
Manchester United, ambayo ilipata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Sheffield United Uwanja wa Old Trafford mwishoni mwa wiki, watamenyana na timu ya Daraja la Kwanza pia, lakini tishio, Derby County.
Arsenal imefika hatua hii baada ya kuitoa Sunderland kwa kuichapa mabao 3-1 Jumamosi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment