• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 23, 2016

  MAN UNITED ‘LA KUVUNDA’, YATANDIKWA 1-0 NYUMBANI NA SOUTHAMPTON

  MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND
  Januari 23, 2016  
  Sunderland 1 - 1 Bournemouth
  Watford 2 - 1 Newcastle United
  West Bromwich Albion 0 - 0 Aston Villa
  Leicester City 3 - 0 Stoke City
  Manchester United 0 - 1 Southampton
  Crystal Palace 1 - 3 Tottenham Hotspur
  Norwich City 4 - 5 Liverpool
  West Ham United 2-2 Manchester City 
  Kesho; Januari 24, 2016
  Everton Vs Swansea City (Saa 10:30 jioni)
  Arsenal Vs Chelsea (Saa 1:00 usiku)

  Mchezaji mpya wa Southampton aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 4, Charlie Austin akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao pekee la ushindi dhidi ya Manchester United PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  BAO pekee la Charlie Austin dakika ya 87 limetosha kuipa ushindi wa ugenini wa 1-0 Southampton dhidi ya Manchester United Uwanja wa Old Trafford jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  Charlie Austin alifunga bao hilo baada ya kutokea benchi akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na James Ward akicheza mechi yake ya kwanza Southampton baada ya kusajiliwa kwa Pauni Milioni 4 akitokea QPR wiki iliyopita.
  Leicester City imejiimarisha kileleni kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Stoke City, mabao ya Daniel Drinkwater dakika ya 42, Jamie Vardy dakika ya 66 na Leonardo Ulloa dakika ya 87 Uwanja wa King Power.
  Sunderland imelazimishwa sare ya 1-1 na Bournemouth, Watford imeifunga 2-1 Newcastle United, West Bromwich Albion imetoka 0-0 na Aston Villa, wakati Tottenham Hotspur imeshinda 3-1 ugenini dhidi ya Crystal Palace mabao ya Harry Kane, Bamidele Alli na Nacer Chadli, wakati la wenyeji limefungwa na Jan Vertonghen aliyejifunga dakika ya 30 Uwanja wa Selhurst Park.
  Liverpool imeshinda 5-4 ugenini dhidi ya Norwich City Uwanja wa Carrow Road. Mabao ya Liverpool yamefungwa na Roberto Firmino mawili, Jordan Henderson, James Milner na Adam Lallana, wakati ya Norwich yamefungwa na Dieudonne Mbokani Bezua, Steven Naismith, Wes Hoolahan na Sebastien Bassong.
  Mchezo kati ya West Ham United na Manchester City unaelekea ukingoni hivi sasa, wakati kesho ligi hiyo itaendelea kwa mechi mbili kati ya Everton na Swansea City kuanzia Saa 10:30 jioni na Arsenal na Chelsea kuanzia Saa 1:00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED ‘LA KUVUNDA’, YATANDIKWA 1-0 NYUMBANI NA SOUTHAMPTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top