• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 24, 2016

  RWANDA YALAMBWA 4-1 NA MOROCCO, IVORY COAST YATINGA ROBO FAINALI

  TIMU ya taifa ya Ivory Coast imefuzu Robo Fainali za Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya kuifunga Gabon mabao 4 -1 Uwanja wa Huye mjini Butare leo.
  Mabao ya Tembo hao yamefungwa na Essis Aka dakika ya 19, Djedje Guiza dakika ya 65, Koffi Boua dakika ya 77 na Ble Treika dakika ya 84wakati la Gabon lilifungwa na Franck Obambou dakika ya 51.

  Franck Djedje Guiza akipambana na Prince Junior Ndinga 

  Mchezo mwingine wa Kundi A, wenyeji Rwanda wamechapwa mabao 4-1 na Morroco, ushindi ambao hata hivyo haukuwazuia Simba wa Atlasi kuipa mkono wa kwaheri michuano hiyo ya tatu.
  Rwanda na Ivory Coast zinafuzu Robo Fainali, wakati Gabon na Morocco safari inaishia hapo. Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Kundi B kati ya Ethiopia na Angola na Cameroon dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RWANDA YALAMBWA 4-1 NA MOROCCO, IVORY COAST YATINGA ROBO FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top