• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 27, 2016

  GUINEA NA TUNISIA ZAENDA ROBO FAINALI, NIGERIA NA NIGER WOTE NJE

  TIMU ya taifa ya Guinea imeifunga Nigeria 1-0 mjini Rubavu Jumanne wakati Tunisia imeikung'uta Niger mabao 5-0 mjini Kigali na timu zote kufuzu Robo Fainali ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) kutoka Kundi C.
  Tunisia imeongoza Kundi kwa wastani wa mabao licha ya kumaliza pointi sawa na Guinea, walioshika nafasi ya pili, wakati Nigeria yenyeb pointi nne imamaliza nafasi ya tatu huku Niger wakishika mkia. 
  Bao pekee lililoibeba Guinea lilifungwa na Ibrahima Sory Sankhon kipindi cha kwanza na sasa NIgeria inarejea nyumbani mapema.

  Mabao ya Tunisia yalifungwa na Saad Bguir mawili, Ahmed Akaichi, Mohamed Ben Amor na Hichem Essifi. 
  Michuano hiyo inaendelea Jumatano kwa mechi za Kundi D kukamilisha hatua ya makundi kwa ujumla. Zambia itamenyana na Mali, wakati Uganda itasaka tiketi ya Robo Fainali mbele ya Zimbabwe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GUINEA NA TUNISIA ZAENDA ROBO FAINALI, NIGERIA NA NIGER WOTE NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top