• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 31, 2016

  ULIMWENGU AENDELEA KUNG’ARA MAZEMBE BILA ‘KAMPANI’ YA SAMATTA

  NYOTA ya Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu (pichani kushoto) imeendelea kung’ara TP Mazembe baada ya jioni ya leo kufunga bao moja katika ushindi wa 4-0 dhidi ya -US Tshinkunku Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, DRC.
  Ulimwengu alifunga bao la kuhitimisha ushindi huo wa mchezo wa Ligi Kuu ya DRC, dakika ya 79 akimalizia pasi ya Mzambia Given Singuluma, ikiwa ni dakika mbili tu tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya Christian Luyindama.
  Mabao mengine ya Mazembe yamefungwa na Christian Luyindama dakika ya 26, Singuluma dakika ya 46 na Giadson Awako dakika ya 73.
  Huu ni mwanzo mzuri wa maisha mapya ya Ulimwengu Mazembe chini ya kocha mpya, Mfaransa Hubert Velud, aliyerithi mikoba ya Patrice Carteron ambaye hakuongezewa Mkataba mapema Januari baada ya kuitumikia klabu hiyo tangu mwaka 2013.
  Aidha, Ulimwengu ameonyesha yuko imara licha ya ‘kumpoteza’ rafiki yake na Mtanzania mwake, Mbwana Ally Samatta waliyecheza naye klabu hiyo kwa miaka minne, ambaye amehamia KRC Genk ya Ubelgiji. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ULIMWENGU AENDELEA KUNG’ARA MAZEMBE BILA ‘KAMPANI’ YA SAMATTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top