• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 24, 2016

  YANGA SC NAO WATINGA 16 BORA MAWINDO YA TIKETI YA CAF 2017

  MATOKEO NA RATIBA KOMBE LA AZAM SPORTS HD – TFF
  Leo; Januari 24, 2016
  Yanga SC 3-0 Friends Rangers (Taifa, Dar es Salaam)
  Njombe Mji 0-0 Prisons (Prisons ameshinda kwa penalti 5-3, Amaan, Njombe)
  Stand Untd 0-1 Mwadui FC (Kambarage, Shinyanga)
  Jana; Januari 23, 2016
  Burkina Faso 0-3 Simba SC (Jamhuri, Morogoro)
  Pamba 1-4 Toto Africans (Kirumba, Mwanza)
  Ndanda FC 5-0 Mshikamno (Nagwanda, Mtwara)
  MECHI ZIJAZO; 
  Januari 25, 2016
  Kagera Sugar Vs Rhino Rangers (Mwinyi, Tabora)
  Panone FC Vs Madini (Ushirika, Moshi)
  African Lyon Vs Azam FC (Karume, Dar es Salaam)
  Januari 26, 2016
  Mtibwa Sugar Vs Abajalo FC (Jamhuri, Morogoro) Lipuli Vs JKT Ruvu (Wambi, Mafinga)
  African Sports Vs Coastal U (Mkwakwani, Tanga)
  Geita Gold Vs Mgambo JKT (Nyankumbu, Geita)
  Januari 27, 2016
  Singida United Vs Mvuvuma (Namfua, Singida)
  Februari 1, 2016
  Wenda FC Vs Mbeya City (Sokoine, Mbeya)
  Paul Nonga (kushoto) akimpongeza Simon Msuva baada ya kufunga bao la pili leo Uwanja wa Taifa

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imefuzu hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports HD TFF Cup baada ya kuichapa mabao 3-0 Friends Rangers jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC inaungana na mahasimu, Simba SC ambao walifuzu jana kwa kuichapa Burkina Faso mabao 3-0 mjini Morogoro.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Elli Sasii aliyesaidiwa na Omary Kambangwa na Shaffih Mohamed wote wa Dar es Salaam, hadi mapumziko, tayari Yanga SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
  Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita, Simon Msuva aliifungia Yanga SC bao la kwanza dakika ya tano akimalizia kona ya Issoufou Boubacar. 
  Msuva tena akafunga bao la pili dakika ya 23 kwa ufundi baada ya kupokea pasi safi ya mshambuliaji Paul Nonga ambaye naye alipenyezewa pasi muruwa ya Salum Telela.
  Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Yanga walipata bao la tatu dk ya 51 likifungwa na mshambuliaji Matheo Anthony kwa kichwa, akimalizia krosi ya Telela.
  Kiungo Haruna Niyonzima (kushoto) akimtoka mchezaji wa Friends Rangers leo Uwanja wa Taifa

  Ikumbukwe bingwa wa michuano hiyo atashiriki Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwakani.
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Salum Telela, Oscar Joshua, Vincent Bossou, Pato Ngonyani, Thabani Kamusoko, Simon Msuva/Deus Kaseke dk68, Haruna Niyonzima/Yussuf Mhilu dk88, Paul Nonga, Matheo Anthony na Issoufou Boubacar/Godfrey Mwashiuya dk70.
  Friends Rangers; Alphonce Raphael, Twalib, Athumani, Mtoro Hamisi, Boniface Nyagawa, Samuel Mathayo, Abbas Wayne, Ally Hamisi, Isihaka Hussein, Good Hamisi/Mgaya JUma dk53, Eleciter Mpepo/Mohammed Banka dk57 na Freddy Cosmas.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC NAO WATINGA 16 BORA MAWINDO YA TIKETI YA CAF 2017 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top