• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 19, 2016

  DAVID HAYE SASA AMTAKA ANTHONY JOSHUA, TENA WAPANDE ULINGONI MWAKA HUU HUU

  David Haye baada ya kurejea kwa kishindo Jumamosi akishinda kwa KO raundi ya kwanza, sasa anamtaka Anthony Joshua PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  BONDIA David Haye amemtaka mpinzani wake katika uzito wa juu, Muingereza mwenzake, Anthony Joshua kuwafurahisha mashabiki kwa kupanda naye ulingoni mwaka huu ‒ lakini ameliita pambano hilo ni la hatari kwa mpinzani wake machachari. 
  Haye alirejea ulingoni usiku wa Jumamosi na kumpiga kwa Knockout (KO) Mark de Mori ndani ya dakika tatu ukumbi wa O2 Arena, London. 
  Bingwa huyo wa zamani wa dunia alikuwa hajapigana kwa miaka mitatu na nusu, lakini akarudi ulingoni kwa staili ya aina yake na kukumbushia enzi zake akitamba katika ndondi za uzito wa juu.
  Kijana wa London mwenye umri wa miaka 35, Anthony Joshua ni bingwa wa uzito wa juu Uingereza

  Mbabe huyo mwenye umri wa miaka 35 anataka kuzipiga na bondia ambaye hajapoteza pambano, Joshua ambaye anakuja kwa kishindo katika medani ya uzito wa juu ya masumbwi.
  "Nataka kurudi (ulingoni) haraka iwezekanavyo. Nataka pambano kubwa. Pambano na Anthony Joshua ndilo ambalo mashabiki wanataka – Nataka kupigana na yule ambaye mashabiki wanataka nipigane naye,".
  "Hilo ndilo pambano ninalolitaka na nina uhakika Anthony Joshua anataka kitu kama hicho. Ni matumaini yangu anakubali unatakiwa kupigana na yule ambaye mashabiki wanataka upigane naye,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DAVID HAYE SASA AMTAKA ANTHONY JOSHUA, TENA WAPANDE ULINGONI MWAKA HUU HUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top