• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 31, 2016

  MALI YAWAGONGA TUNISIA 2-1 NYAMIRAMBO, SASA KUMENYANA NA IVORY COAST NUSU FAINALI

  TIMU ya taifa ya Mali imeifunga Tunisia mabao 2-1 katika mchezo mkali na wa kusisimua wa Robo Fainali ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda.
  Kwa ushindi huo Mali inatinga Nusu Fainali ya CHAN 2016 ambako itamenyana na Ivory Coast Februari 4 Saa 10:00 jioni Uwanja wa Amahoro mjini Kigali.

  Mohammed Ali Monser alimalizia pasi nzuri ya Saad Bguir kuifungia Tunisia bao la kuongoza dakika ya 14, kabla ya Mali kusawazisha kupitia kwa Abdoulaye Diarra.
  Aliou Dieng akaifungia Mali bao la ushindi kwa penalti baada ya refa Hamada El Moussa Nampiandraza kuwazawadi tuta kufuatia beki wa Tunisia, Zied Boughattas kuunawa mpira kwenye boksi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALI YAWAGONGA TUNISIA 2-1 NYAMIRAMBO, SASA KUMENYANA NA IVORY COAST NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top