• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 27, 2016

  KIPRE TCHETCHE AINUSURU AZAM KUZAMA KWA ZESCO, AISAWAZISHIA BAO DAKIKA YA MWISHO

  Kipre ameinusuru Azam kuzama kwa Zesco
  AZAM FC imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Zesco United mchana wa leo katika mchezo wa michuano maalum Uwanja wa Levy Mwanawaswa mjini Ndola, Zambia.
  Katika mchezo huo uliochezwa kwenye mvua, Zesco walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Jesse Were dakika ya kwanza tu.
  Azam FC ilisota hadi mwishoni mwa kipindi cha pili ilipofanikiwa kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche dakika ya 90.  
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Waziri Salum/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk67, David Mwantika, Serge Wawa, Erasto Nyoni, Jean Baptiste Mugiraneza, Himid Mao/Kipre Balou dk46, Frank Domayo, John Bocco/Allan Wanga dk67 na Kipre Tchetche.
  Mchezo mwingine wa michuano hiyo, wenyeji wengine Zanaco wamelazimishwa sare ya 2-2 Chicken ya Zimbabwe.
  Zanaco ilipata mabao yake kupitia kwa Roderick Kabwe na Fashion Sakala, wakati ya Chicken Inn yalifungwa na Brian Juru na Obidiah Tarumbwa.

  Zesco itacheza na Zanaco kesho, wakati Azam itacheza na Chicken Inn.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIPRE TCHETCHE AINUSURU AZAM KUZAMA KWA ZESCO, AISAWAZISHIA BAO DAKIKA YA MWISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top