• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 29, 2016

  SAFARI YA RWANDA MWISHO KESHO CHAN?

  ROBO Fainali za Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika zinachezwa kesho na keshokutwa Rwanda.
  Wenyeji Rwanda watakuwa wana kazi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Uwanja wa Amahoro mjini Kigali, wakati Cameroon itamenyana na Ivory Coast.
  Jumapili hatua ya Robo Fainali itahitimishwa kwa michezo kati ya Tunisia na Mali na Zambia na
  Guinea.
  Wenyeji Rwanda wanatarajiwa kupata wakati mgumu mbele ya DRC, mabingwa wa kwanza wa michuano hiyo mwaka 2009 nchini Ivory Coast.
  Rwanda wana mtihani mzito mbele ya DRC kesho CHAN 

  Na hiyo inatokana na ukweli kwamba kwa maana ya timu na hata kiwango cha mchezaji mmoja mmoja, DRC ni zaidi ya Rwanda.
  Lakini morali ya hali ya juu ndani ya kikosi cha Nyigu wa Rwanda inatarajiwa kuwa silaha kuu katika mchezo wa kesho dhidi Kongo.
  Cameroon na Ivory Coast ni mchezo ambao lolote linaweza kutokea kama ilivyo kwa mchezo kati ya Tunisia na Mali, wakati Zambia inapewa nafasi ya kuitoa Guinea.  
  Hatari moja inayoinyemelea michuano hiyo ni kupoteza watazamaji iwapo wenyeji, Rwanda watatolewa kesho na DRC, kwani mashabiki wa nyumbani hawatahudhuria mechi tena kwa wingi kama wakati timu yao ikiwa mashindanoni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAFARI YA RWANDA MWISHO KESHO CHAN? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top