• HABARI MPYA

    Sunday, January 31, 2016

    GUINEA YAITUPA NJE ZAMBIA KWA MATUTA, SASA KUIVAA DRC NUSU FAINALI

    TIMU ya taifa ya Guinea imefanikiwa kuitoa Zambia katika michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya kuifunga kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Umuganda. Gisenyi.
    Nahodha Chris Katongo alikosa penalti ya kwanza, kabla ya Stephen Kabamba na Daut Musekwa kukosa pia, wakati waliofunga penalti za Chipolopolo ni Buchizya Mfune, Spencer Sautu, Clatous Chama na Adrian Chama.
    Penalti za Guinea zimefungwa na Ibrahima Sory Bangoura, Mohamed Thiam, Issiaga Camara, Ibrahima Sory Soumah na Abdul Aziz Keita, wakati Ibrahima Sory Sankhon na Mohamed Youla walikosa.

    Mchezo uliotangulia, Mali imeifunga Tunisia mabao 2-1 Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda na sasa itamenyana na Ivory Coast Februari 4 Saa 10:00 jioni Uwanja wa Amahoro mjini Kigali, wakati Guinea itamenyana na DRC.
    Mohammed Ali Monser alimalizia pasi nzuri ya Saad Bguir kuifungia Tunisia bao la kuongoza dakika ya 14, kabla ya Mali kusawazisha kupitia kwa Abdoulaye Diarra.
    Aliou Dieng akaifungia Mali bao la ushindi kwa penalti baada ya refa Hamada El Moussa Nampiandraza kuwazawadi tuta kufuatia beki wa Tunisia, Zied Boughattas kuunawa mpira kwenye boksi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GUINEA YAITUPA NJE ZAMBIA KWA MATUTA, SASA KUIVAA DRC NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top