• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 27, 2016

  UGANDA ‘WEUPE KINOMA’, WATOLEWA MAPEMAAA CHAN

  UGANDA itapanda ndege mapema kesho kurejea nyumbani, Kampala baada ya kutupwa nje ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN).
  Korongo wa Kampala wametoa sare ya 1-1 na Zimbabwe katika mchezo wa mwisho wa Kundi D leo mjini Kigali, Rwanda na hivyo wanamaliza na pointi mbili.
  Zambia imemaliza na pointi saba baada ya sare ya 0-0 na Mali leo waliomaliza na pointi tano, ambao kwa pamoja wanakwenda Robo Fainali, huku Zimbabwe ikiungana na Uganda kuaga CHAN ya 2016.

  Na katika mchezo wa leo, chupuchupu Uganda ilale kama si Geoffrey Sserunkuma kuisawazishia bao dakika ya nne ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida, kufuatia William Manondo kuanza kuifungia Zimbabwe dakika ya 49.
  Mechi za makundi zimefikia tamati leo na timu zilizofuzu hatua ya kwanza ya mtoano ni Rwanda, Ivory Coast (Kundi A), Cameroon, DRC (Kundi B), Tunisia na Guinea za Kundi C zinazoungana na Zambia na Mali za Kundi D.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UGANDA ‘WEUPE KINOMA’, WATOLEWA MAPEMAAA CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top