• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 25, 2016

  CAMEROON YATINGA ROBO FAINALI CHAN, ANGOLA 'YAIOTEA' ETHIOPIA 2-1

  TIMU ya taifa ya Cameroon imetinga Robo Fainali ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya DRC jioni ya leo mjini Kigali, Rwanda.
  Kwa ushindi huo, Cameroon inamaliza kileleni mwa Kundi B baada ya kufikisha pointi saba kutokana na kushinda dhidi ya DRC na Angola na kutoa sare na Ethiopia. DRC imefuzu kama mshindi wa pili wa kundi hilo baada ya kuzifunga Angola na Ethiopia. 
  Mabao ya Cameroon yamefungwa na Nlend Samuel, Moumi Ngamaleu Nicolas Brice na Yazid Atouba Emane, wakati la DRC limefungwa na Jean Marc Makusu.
  Cameroon imefuzu Robo Fainali Kombe la CHAN baada ya kuifunga DRC 3-1

  Mchezo mwingine wa kundi hilo leo, mabao mawili ya Manuel David Afonso yameipa ushindi wa 2-1 Angola dhidi ya Ethiopia Uwanja wa Amahoro leo.
  Afonso alifunga mabao yake katika dakika za 54 na 75, wakati la Ethiopia limefungwa na Seyoum Tesfaye dakika ya 77.
  Pamoja na ushindi huo, Angola inaungana na Ethiopia kufungasha virago vyao kurejea nyumbani wakiipa mkono wa kwaheri CHAN ya mwaka huu, DRC na Cameroon zikifuzu Robo Fainali kutoka kundi hilo.
  Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za mwisho za Kundi C, Guinea ikimenyana na Nigeria na Tunisia ikivaana na Niger.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAMEROON YATINGA ROBO FAINALI CHAN, ANGOLA 'YAIOTEA' ETHIOPIA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top