• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 31, 2016

  16 BORA KOMBE LA FA ENGLAND, MAN UNITED WAPEWA VIBONDE, CHELSEA NA MAN CITY, ARSENAL...

  Kocha wa Man United, Louis Van Gaal
  TIMU ya Chelsea imepangwa kumenyana na Manchester City katika Raundi ya Tano ya Kombe la FA Cup baada ya kuitoa MK Dons.  
  Manchester United wamepangiwa timu ya Daraja la Kwanza, Shrewsbury Town, wakati Arsenal walioshinda Kombe la FA misimu miwili mfululizo iliyopita watamenyana na Hull City, timu ambayo waliifunga kutwaa taji hilo mwaka 2014.  
  Liverpool na West Ham wanatarajiwa kumenyana katika mchezo wa marudiano baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa Anfield Jumamosi na mshindi ataifuata na Blackburn Rovers.
  Tottenham itakuwa mwenyeji wa Crystal Palace Uwanja wa White Hart Lane, Reading itamenyana na mshindi wa mechi ya marudiano kati ya West Brom na Peterborough wakati Leeds itasafiri kuwafuata Watford na Bournemouth itamenyana na Everton Uwanja wa Vitality.  

  RATIBA KAMILI HATUA YA 16 BORA KOMBE LA FA ENGLAND: 

  Chelsea vs Manchester City
  Reading vs West Brom/Peterborough
  Watford vs Leeds
  Shrewsbury vs Manchester United
  Blackburn vs Liverpool/West Ham
  Tottenham vs Crystal Palace
  Arsenal vs Hull
  Bournemouth vs Everton
  (Mechi zitachezwa wikiendi ya Februari 19) 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: 16 BORA KOMBE LA FA ENGLAND, MAN UNITED WAPEWA VIBONDE, CHELSEA NA MAN CITY, ARSENAL... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top