• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 18, 2016

  MALINZI APATA UGENI MZITO TFF, RAIS WA SOKA YA ASIA ATUA DAR

  RAIS wa Shirikisho la Soka Asia (AFC) na Makamu wa Rais wa FIFA, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa amewasili nchini leo mchana na kupokelewa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.
  Sheikh Salman amekuja nchini kwa matembezi ya siku ya mbili na atakua na mwenyeji wake Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
  Kesho Jumanne, Sheikh Salman Bin Ebrahim Ali Khalifa atamtembelea ofisini Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel.
  Malinzi (kulia) akiwa na Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa baada ya kumpokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). Dar es Salaam leo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALINZI APATA UGENI MZITO TFF, RAIS WA SOKA YA ASIA ATUA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top