• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 23, 2016

  SIMBA SC YATINGA 16 BORA MAWINDO YA TIKETI YA KOMBE LA CAF 2017

  RATIBA KOMBE LA AZAM SPORTS HD – TFF
  Januari 23, 2016
  Burkina Faso 0-3 Simba SC (Jamhuri, Morogoro)
  Pamba 1-4 Toto Africans (Kirumba, Mwanza)
  Ndanda FC 5-0 Mshikamno (Nagwanda, Mtwara)
  Januari 24, 2016
  Yanga SC Vs Friends Rangers (Taifa, Dar es Salaam)
  Njombe Mji Vs Prisons (Amaan, Njombe)
  Stand Untd Vs Mwadui FC (Kambarage, Shinyanga)
  Januari 25, 2016
  Kagera Sugar Vs Rhino Rangers (Mwinyi, Tabora)
  Panone FC Vs Madini (Ushirika, Moshi)
  African Lyon Vs Azam FC (Karume, Dar es Salaam)
  Januari 26, 2016
  Mtibwa Sugar Vs Abajalo FC (Jamhuri, Morogoro) Lipuli Vs JKT Ruvu (Wambi, Mafinga)
  African Sports Vs Coastal U (Mkwakwani, Tanga)
  Geita Gold Vs Mgambo JKT (Nyankumbu, Geita)
  Januari 27, 2016
  Singida United Vs Mvuvuma (Namfua, Singida)
  Februari 1, 2016
  Wenda FC Vs Mbeya City (Sokoine, Mbeya)
  Hamisi Kiiza (kulia) amefunga mabao mawili Simba SC ikishinda 3-0 na kutinga 16 Bora ya Kombe la TFF 

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  SIMBA SC imefuzu Raundi ya Nne ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports HD TFF Cup baada ya kuwachapa wenyeji Burkina Faso mabao 3-0 jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
  Shujaa wa Simba SC inayokwenda hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo ambayo itatoa mwakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwakani, alikuwa ni mshambuliaji Mganda, Hamisi Friday Kiiza aliyefunga mabao mawili, wakati lingine limefungwa na kiungo Said Ndemla. 
  Kiiza alifunga mabao yake dakika ya 77 kwa shuti kali akimalizia krosi ya Abdi Banda na la tatu dakika ya 90 kwa penalti, baada ya kiungo Said Ndemla kuangushwa kwenye boksi.
  Ndemla alifunga bao la pili la Simba SC hii leo dakika ya 89 kwa shuti la umbali wa mita 38, bao lililowasisimua zaidi mashabiki uwanjani. 
  Mapema kipindi cha kwanza, Simba SC ilipoteza nafasi mbili nzuri za mabao, kwanza dakika ya 11 wakati winga Joseph Kimwaga alipowalamba chenga vizuri mabeki wa Burkina Faso, lakini akapiga nje na dakika ya 39 beki Mrundi, Emery Nimubona alipopiga nje akiwa karibu na lango. Burkina Faso nayo iliyoongozwa na mkongwe, Ulimboka Alfred Mwakingwe aliyewahi kuwika Simba SC ilipoteza nafasi pia.
  Dakika ya 39 Ulimboka alimdakisha kipa Muivory Coast wa Simba SC, Vincent Angban shuti dhaifu akiwa kwenye nafasi nzuri na dakika nne baadaye akachelewa kupiga akiwa kwenye boksi, hadi mabeki wakaokoa.
  Katika mechi nyingine za michuano hiyo leo, Toto Africans imeifunga 4-1 Pamba Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, wakati Ndanda FC imeifunga 5-0 Mshikamano Uwanja wa Nagwanda SIjaona mjini Mtwara.
  Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi tatu pia, Yanga SC na Friends Rangers Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mji Njombe na Prisons Uwanja wa Amaan, Njombe na Stand United na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa: Vincent Angban, Hassan Kessy, Abdi Banda, Novaty Lufunga, Jonas Mkude, Emery Nimubona/Mwinyi Kazimoto dk66, Said Ndemla, Hamisi Kiiza, Mussa Mgosi/Danny Lyanga dk46 na Joseph Kimwaga/Hajji Ugando dk29.
  Burkina Faso: Hashim Nzota, Kessy Kessy, Anthony Matangalu, Zawadi Mauya, Hussein Shehe, Victor Mswaki, Sharif Mohammed, Jonathan Kishimba/Jumanne Wida dk69, Ulimboka Mwakingwe na Hassan Mkota/Athumani Mohammed dk46. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATINGA 16 BORA MAWINDO YA TIKETI YA KOMBE LA CAF 2017 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top