• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 27, 2016

  HAJIB AWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI DESEMBA SIMBA SC

  MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Ibrahim Hajib ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Desemba wa klabu hiyo.
  Hajib (pichani kushoto) ameshinda tuzo hiyo ambayo huambatana na kitita cha Sh. 500,000 baada ya kufunga mabao matano mwezi uliopita na kuisaiia klabu hiyo kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Kwa sasa Hajib anakosekana Simba SC kutokana na kuwa majeruhi baada ya kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar wiki iliyopita, kufuatia kugongwa na Nahodha wa zamani wa Wekundu hao wa Msimbazi, Henry Joseph.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HAJIB AWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI DESEMBA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top