• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 21, 2016

  DRC YATINGA ROBO FAINALI CHAN 2016, ETHIOPIA WATOKA 0-0 NA CAMEROON

  JAMHURI ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imefanikiwa kufuzu Robo Fainali ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Angola.
  Kwa matokeo hayo pia, Angola inaaga michuano hiyo inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
  Mabao ya DRC yamefungwa na Nelson Munganga, Mechak Elia, Jonathan Bolingi na Merveille Bokadi, wakati ya Angola yamefungwa na Jacinto Dala ‘Gelson’ na Joel Kimwaki aliyejifunga.
  Mchezo mwingine wa kundi hilo, Cameroon imelazimishwa sare ya 0-0 na Ethiopia na sasa italazimika kusubiri hadi mechi yake ya mwisho kuangalia uwezekano wa kwenda Robo Fainali.
  Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Kundi C, Tunisia dhidi ya Nigeria na Niger dhidi ya Guinea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DRC YATINGA ROBO FAINALI CHAN 2016, ETHIOPIA WATOKA 0-0 NA CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top