• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 31, 2016

  MGAMBO JKT YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA NDANDA FC MKWAKWANI

  MATOKEO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Januari 30, 2016
  Coastal Union 2-0 Yanga SC
  Simba SC 4-0 African Sports
  JKT Ruvu 0-0 Majimaji
  Mtibwa Sugar 1-0 Stand United
  Mwadui FC 1-0 Toto Africans
  Januari 31, 2016
  Mgambo JKT 1-1 Ndanda FC
  Kagera Sugar 2-0 Mbeya City
  Mgambo JKT wamelazimishwa sare ya 1-1 na Ndanda FC leo Uwanja wa Mkwakwani

  Na Salma Isihaka, TANGA
  MGAMBO Shooting imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Ndanda FC ya Mtwara katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
  Matokeo hayo, yanaifanya Mgambo JKT ifikishe pointi 17 baada ya kucheza mechi 16 na kuendelea kukaa nafasi ya tisa, wakati Ndanda FC inafikisha pointi 13 baada ya kucheza mechi 16, pia wakiendelea kukaa nafasi ya 14 katika Ligi ya timu 16 ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka.
  Chande Magoja alianza kuifungia Mgambo JKT dakika ya 51, kabla ya Omar Mponda kuisawazishia Ndanda FC dakika ya 77.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu jana, Coastal Union waliifunga 2-0 Yanga SC Mkwakwani, Simba SC iliitandika 4-0 African Sports Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, JKT Ruvu ilitoka sare ya 0-0 na Majimaji Uwanja wa Karume, Mtibwa Sugar ikashinda 1-0 dhidi ya Stand United na Mwadui FC ikashinda 1-0 dhidi ya Toto Africans.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MGAMBO JKT YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA NDANDA FC MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top