• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 23, 2016

  SARE ZATAWALA KUNDI C, NIGERIA 1-1 NA TUNISIA, NIGER 2-2 NA GUINEA

  TIMU ya taifa ya Tunisia imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na Nigeria katika mchezo wa Kundi C Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee jana mjini Kigali, Rwanda.
  Super Eagles, ambao walihitaji ushindi kwenda Robo Fainali, walikuwa wa kwanza kupata bao kupiyia kwa Chisom Chikatara dakika ya 51, kabla ya Tunisia kupata bao lililokataliwa dakika ya 44 kwa sababu mfungaji, Ahmed Akaichi alikuwa amezidi.
  Ahmed Akaichi amefunga mabao mawili jana moja likikataliwa
  Lakini mshambuliaji huyo aliyefunga mabao mawili dhidi ya Guinea katika mchezo wa kwanza Jumatatu, akaifungia tena Tunisia kuisawazishia dakika ya 60.
  Mchezo mwingine wa kundi hilo, Niger na Guinea zimetoa sare ya 2-2 na kufanya timu za kwenda Robo Fainali zipatikate katika mechi za mwisho.
  Mabao ya Niger yamefungwa na Youssef Alio dakika ya 36 na Adamou Musaminutes dakika ya 49, wakati ya Guinea yamefungwa na Aboubacar Sylla dakika ya 37 na Aboubakar Bangoura dakika ya 75.
  Nigeria sasa ina pointi nne na itahitaji kuwafunga Guinea wanaoshika nafasi ya pili Jumanne ili kufuzu Robo Fainali kama vinara wa kundi.
  Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi za Kundi D, Zimbabwe ikimenyana na Mali na Uganda na Zambia Uwanja wa Rubavu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SARE ZATAWALA KUNDI C, NIGERIA 1-1 NA TUNISIA, NIGER 2-2 NA GUINEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top