• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 22, 2016

  MASCHERANO AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MIWILI KWA KUKWEPA KODI

  BEKI Javier Mascherano amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela na kupigwa faini ya Euro 815,000 kwa kukutwa na hatia mbili za kukwepa kodi.
  Pamoja na hayo, nyota huyo wa Barcelona hataki kwenda kutumikia kifungo hicho jela, baada ya Mwanasheria wake, David Aineto kuomba kifungo cha jela kigeuzwe kuwa faini, ambayo tayari amelipa.
  Mwanasheria wa Mascherano pia anapambana kuondoa rekodi ya ukwepaji kodi kwa mteja wake kwa kulipa faini zaidi.
  Javier Mascherano akiondoka mahakama ya Barcelona jana baada ya kukiri makosa mawili ya ukwepaji kodi PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Nchini Hispania watu wanaohukumiwa kifungo kisichozidi miaka miwili jela, huruhusiwa kulipa faini ili wasiende jela, labda wawe wamehukumiwa kwa makosa ya jinai.
  Mascherano, mwenye umri wa miaka 31, alihukumiwa kifungo cha miezi minne na miezi miezi minane kwa makosa mawili aliyoyafanya mwaka 2011 na 2012.
  Nyota huyo wa Argentina tayari amelipa kiasi cha kodi anachodaiwa kukwepa Euro Milioni 1.6 kabla ya kupewa adhabu hiyo. Mascherano pia amelipa ziada ya fedha hizo, lakini bado ametozwa faini.
  Makosa yake ya ukwepaji kodi ni kutokana na kushindwa kuainisha vipato vyake vingine kutonana na haki za matumizi ya picha zake ambazo zinamilikiwa na kampuni za Ureno na Marekani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MASCHERANO AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MIWILI KWA KUKWEPA KODI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top