• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 24, 2016

  NGASSA AENDELEA KUWASHIKA AFRIKA KUSINI, AIONGOZA TENA FREE STATE KUTOA ADHABU ABSA

  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa (pichani kushoto) ameendelea kuwa sehemu ya mafanikio ya klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini baada ya jana kuwamo katika kikosi kilichoifunga Bloemfontein Celtic 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Absa Uwanja wa Goble Park mjini Bethelehem.
  Bao pekee la timu ya Ngassa jana lilifungwa na Lucky Mohomi dakika ya 22, huo ukiwa ushindi wa kwao Ea Lla Koto mwaka 2016. Ngassa alicheza kwa dakika 62 kabla ya kumpisha Venter.
  Free State sasa imepanda hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, ikifikisha pointi 21 baada ya kucheza mechi 14, ikizidiwa wastani wa mabao tu na Golden Arrows wanaoshika nafasi ya tano.
  Aidha, FS inazidiwa pointi nne na Kaizer Chiefs iliyo nafasi ya nne, wakati Black Aces ina pointi 30 katika nafasi ya tatu, Bidvest Wits pointi 32 katika nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi 15 sawa na vinara, Mamelodi Sundowns wenye pointi 33.
  Kikosi cha Free State Stars jana kilikuwa: Diakite, Nkausu, Thlone, Chabalala, Sankara, Sekola/Makhaula dk87, Masehe, Mashego, Mohomi, Fileccia/Japhta dk21 na Ngassa/Venter dk62.
  Bloemfontein Celtic: Tignyemb, Fransman, Matuka, Rikhotso, Nyatama, Morena, Shikweni/Lakay dk83, Jooste/Lamola dk54, Ndengane, April na Massa/Zuma dk68.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGASSA AENDELEA KUWASHIKA AFRIKA KUSINI, AIONGOZA TENA FREE STATE KUTOA ADHABU ABSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top