• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 30, 2016

  AZAM FC YANG’ARA ZAMBIA, YAWATANDIKA MABINGWA WA ZIMBABWE 3-1

  John Bocco ameifunga bao Azam leo Ndola
  AZAM FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chikeck Inn ya Zimbabwe katika mchezo wa michuano maalum ya kirafiki mchana wa leo Uwanja wa Levy Mwanawaswa mjini Ndola, Zambia.
  Ushindi huo unaifanya Azam FC sasa iongoze katika michuano hiyo inayoshirikisha timu nne, baada ya kufikisha pointi nne, kufuatia kutoa sare ya 1-1 na Zesco United katika mchezo wake wa kwanza Jumatano.
  Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na Nahodha John Bocco dakika ya 31, Kipre Tchetche dakika ya 54 kwa penalti wakati bao la tatu walijifunga wenyewe mabingwa wa Zimbabwe dakika ya 67. 
  Mchezo kati ya Zesco United na Zanaco FC ndiyo unafutaia sasa Uwanja wa Levy Mwanawaswa, wakati mechi za mwisho zitachezwa Jumatano.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Manula Aishi, Erasto Nyoni, Ramadhani Singano, Abdallah Kheri, Pascal Wawa, Himid Mao, Mudathir Yahya, Kipre Bolou, Shomary Kapombe/Said Mourad dk85, John Bocco/Kipre Tchetche dk46 na Ame Ali/Allan Wanga dk46.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YANG’ARA ZAMBIA, YAWATANDIKA MABINGWA WA ZIMBABWE 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top