• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 30, 2016

  REAL YASAJILI WINGA MZAMBIA, ATAMBULISHWA RASMI HISPANIA TAYARI KWA KAZI

  KLABU ya Real Betis imemsajili kwa mkopo wa hadi mwishoni mwa msimu, kiungo chipukizi wa Chelsea, Charly Musonda. 
  Dogo huyo wa umri wa miaka 19, akiwa na The Blues ameshinda mataji ya vijana ya Ligi Kuu ya U-21, Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la FA, lakini hakupata nafasi ya kuchezea kikosi cha kwanza cha Chelsea chini ya kocha Mreno, Jose Mourinho.
  Musonda alifanya mazungumzo na kocha wa muda wa Chelsea, Guus Hiddink kuangalia kama ataingia kwenye mipango ya Mholanzi huyo na pande zote mbili zikafikia makubaliano ya kwenda kucheza kwa mkopo kupata uzoefu. 

  Charly Musonda (katikati) amejiunga na Real Betis ya Hispania kwa mkopo kutoka Chelsea  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Mchezaji huyo wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Ubelgiji amesema: "NIna furaha sana kuwa hapa na ninavutiwa kuanza. Binafsi nataka kufanya vizuri, kwa timu na kwa mashabiki,".
  Feyenoord, AZ Alkmaar na QPR zote zilikuwa zinamtaka kinda huyo mwenye kipaji, lakini akachagua kwenda Hispania katika timu ambayo inashika nafasi ya 14 kwa sasa kwenye La Liga, ikibebwa na pointi nne tu kuangukia kwenye nafasi ya kushuka daraja.
  Baada ya kupandishwa kikois cha kwanza kufuatia kufanya vizuri akiwa na U-21, winga alijikuta anakosa raha kwa kutopata namba kikosi cha kwanza na atajaribu bahati yake Hispania. 
  Mtoto huyo wa kiungo wa zamani wa Anderlecht ya Ubelgiji na timu ya taifa ya Zambia, Charly Musonda Sr, Musonda aliichezea kikosi cha kwanza cha Chelsea wakati wa mechi za kujiandaa na msimu na akawavutia wengi Stamford Bridge. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL YASAJILI WINGA MZAMBIA, ATAMBULISHWA RASMI HISPANIA TAYARI KWA KAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top