• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 19, 2016

  NAHODHA KORONGO WA UGANDA ASEMA; "LENGO LETU NUSU FAINALI"

  TIMU ya taifa ya Uganda inamenyana na Mali katika mchezo wake wa kwanza wa Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mjini Kigali, Rwanda leo na Nahodha wake, Farouk Miya amesema lengo lao la kwanza ni kufika Nusu Fainali.
  Korongo wa Uganda ambao wapo nafasi ya 62 katika viwango vys ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ambayo ni nafasi ya juu zaidi kwao kihistoria, wapo Kundi D pamoja na Mali, Zimbabwe na Zambia.
  Na kinda wa miaka 19, Miya ambaye hivi karibuni ameisaidia The Cranes kutwaa kutwaa taji la 14 la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mjini Ethiopia, amesema; "Lengo letu ni kufika Nusu Fainali" amesema Mwanasoka huyo Bora wa Uganda.
  Nahodha wa Uganda, Farouk Miya amesema lengo lao ni kufika Nusu Fainali CHAN 2016

  Miya amesema kwamba ni vizuri wanapewa nafasi kutokana na mafanikio ya karibuni, lakini hataki kuamini kwamba takwimu bila kujituma zinaweza kuleta matokeo mazuri. "Tunatakiwa kukabiliana na mpinzani yeyote na kujituma ili kushinda mechi, kwa lengo la kutimiza azma yetu ya kufika Nusu Fainali,"amesema.
  Miya amesema katika kundi lao, wanaihofia zaidi ya Zambia, kwa sababu; "Timu zote ni nzuri, lakini zaidi ni Zambia kwa sababu wanawajua wachezaji wetu wengi na tumekutana nao mara nyingi kuliko timu nyingine. Tunazipa uzito ule ule timu zote na tutapambana kwa bidii katika kila mechi,"amesema.
  Mzunguko wa kwanza wa CHAN unatarajiwa kufikia tamati leo kwa mechi za Kundi D, Zimbabwe ikianza kumenyana na Zambia kabla ya Uganda kupepetana na Mali.
  Farouk Miya ni Mwanasoka Bora wa Uganda 2015 na hapa ni wakati amepokea tuzo yake 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NAHODHA KORONGO WA UGANDA ASEMA; "LENGO LETU NUSU FAINALI" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top