• HABARI MPYA

    Sunday, December 13, 2015

    NGASSA AWAKOSAKOSA UNIVERSITY OF PRETORIA, SARE 1-1 NA FREE STATE

    NYOTA wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa (pichani kushoto) amecheza dakika zote 90 leo timu yake, Free State Stars ikilazimishwa sare ya 1-1 na University of Pretoria katika mchezo wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini Uanja wa Goble Pakr mjini Bathelehem.
    Danny Venter alianza kuifungia Free State dakika ya 36, kabla ya Lennox Bacela kuisawazishia University of Pretoria dakika ya 57.
    Awali ya hapo, mapema tu dakika ya saba Ngassa alikaribia kufunga baada ya kufumua shuti kali lililopaa juu ya lango, huku mashabiki wa Free State wakiinuka kutaka kushangilia kabla ya kusikitika.
    Kikosi cha Free State Stars kilikuwa; Diakite, Masehe, Mashego, Chabalala, Shabalala, Thebakang/Thlone dk46, Ngassa, Sekola, Fileccia/Thetani dk70, Vilakazi na Venter/Japhta dk82.
    University of Pretoria: Arubi, Mwedihanga, Monyai, Jaure, Sibande, Ntombayithethi/Mosadi dk46, Mathosi/Kebede dk46, Zwane, Maruping, Mnyamane na Bacela/Nkoana dk75.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGASSA AWAKOSAKOSA UNIVERSITY OF PRETORIA, SARE 1-1 NA FREE STATE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top