• HABARI MPYA

    Tuesday, November 11, 2014

    STARS YAPAA ‘SAUZI’ KUWEKA KAMBI KABLA YA KWENDA KUIVAA SWAZILAND

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimeondoka alfajiri ya leo kwenda Afrika Kusini kuweka kambi ya siku mbili kabla ya kwenda Swziland Novemba 13, mwaka huu.
    Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ameondoka na wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16, mwaka huu mjini Mbabane.
    Kikosi hicho kiliingia kambini Saa 6:00 mchana wa jana kwenye hoteli ya Accomondia, kabla ya jioni yake kufanya mazoezi kwenye gym.
    Amri Kiemba yumo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichokwenda Afrika Kusini

    Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni makipa Aishi Manula (Azam) na Deogratias Munishi (Yanga). Mabeki ni Abubakar Mtiro (Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam), Emmanuel Simwanda (African Lyon), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr Joshua (Yanga), Said Moradi (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari Kapombe (Azam).
    Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Haruna Chanongo (Simba), Himid Mao (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Said Ndemla (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
    Washambuliaji ni Juma Luizio (ZESCO, Zambia), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo).
    Mara ya mwisho, Stars iliifunga 4-1 Benin katika mchezo wa kirafiki unaotambuliwa na FIFA pia, Oktoba 12, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS YAPAA ‘SAUZI’ KUWEKA KAMBI KABLA YA KWENDA KUIVAA SWAZILAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top