• HABARI MPYA

  Thursday, November 20, 2014

  BALAA JUU YA BALAA MAN UNITED, FALCAO APATA MAUMIVU MAPYA

  KOCHA Louis van Gaal ameendelea kuogelea kwenye wimbi la matatizo baada ya leo kugundulika mshambuliaji wa Manchester United, Radamel Falcao atakuwa nje ya Uwanja kwa angalau wiki mbili nyingine katakana na kupata maumivu mapya.
  Falcao amekuwa na mwanzo mgumu katika klabu hiyo tangu atue katika siku ya mwisho ya kufunga pazia la usajili kwa mkopo kutoka Monaco.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye ni miongoni mwa nyota wanaolipwa mishahara mikubwa Old Trafford, amefunga bao tu hadi sasa na hajafanikiwa kucheza kwa dakika zote 90 kwa Mashetani hao Wekundu.
  Radamel Falcao (right) pictured in action for Manchester United against West Ham in September
  Radamel Falcao (kulia) akiichezea Manchester United dhidi ya West Ham Septemba 
  Falcao (left) was unveiled with Daley Blind (right) on arrival at Old Trafford - both are now injured
  Falcao (kushoto) akiwa na Van Gaal na Daley Blind (kulia) wakati wa kutambulishwa kwao baada ya kutua Old Trafford - wote ni majeruhi

  Falcao hajaichezea United kwa mwezi sasa katakona na maumivu ya ndama na sasa ameumia tena baada ya kuthibitishwa leo mchana.
  'Van Gaal ameiambia #MUTV kwamba @Falcao 'ana maumivu mapya' na atahitaji angalau wiki mbili kurejea kwenye kikosi cha kwanza. #mufc,' imeandikwa kwenye ukurasa wa Twitter wa Man United.
  Tangu atue, Falcao amecheza mechi tano tu kwa Mashetani hao Wekundu na kufunga bao moja tu dhidi ya Everton mwezi Oktoba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BALAA JUU YA BALAA MAN UNITED, FALCAO APATA MAUMIVU MAPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top