• HABARI MPYA

  Thursday, November 27, 2014

  MSIBA SIMBA SC, IVO AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KIPA wa Simba SC, Ivo Mapunda amefiwa na mama yake mzazi, Igasia Nchimbi jana usiku.
  Kipa huyo nambari moja wa Wekundu wa Msimbazi, ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mama huyo amefia wilayani Tukuyu mjini Mbeya usiku wa jana akiwa ana umri wa miaka 75.
  “Mama amefariki jana, baada ya kusumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na hivi nipo Mbeya kwa taratibu za mazishi,”amesema Ivo.
  Pole kipa; Ivo Mapunda amefiwa na mama yake mzazi jana usiku

  Kifo cha mama yake huyo, kinamfanya Ivo sasa awe amepoteza wazazi wake wote wawili, kufuatia kifo cha baba yake, Philip Mapunda Februari mwaka huu, aliyefia pia Tukuyu Mbeya.
  Mzee Mapunda aliyekuwa ana umri wa miaka 86 alifariki akiwa katika hospitali ya Ikonda, iliyopo Njombe ambako alikuwa amelazwa kwa takriban miezi miwili na nusu kwa maradhi ya kibofu cha mkojo, sukari na vidonda vya tumbo.  Pole Ivo na familia yake. Mungu ampumzishe kwa amani Bi Igasia Nchimbi.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSIBA SIMBA SC, IVO AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top