• HABARI MPYA

    Sunday, November 23, 2014

    MANNY PACQUIAO AMTWANGA CHRIS ALGIERI ALIYEKUWA HAJAPIGWA HATA MARA MOJA KABLA

    BONDIA Manny Pacquiao wa Ufilipino, amefanikiwa kutetea taji lake la WBO uzuto wa Welter, baada ya kumshinda kwa pointi Chris Algieri katika pambano lililomalizika muda huu mjini Macau, China. 
    Pacquiao ameshinda kwa pointi za majaji wote, wa kwanza akitoa 119 kwa 103, wa pili 119 kwa 103 na wa tatu 120 kwa 102.
    Hilo linakuwa pambano la kwanza kwa Algieri kupoteza baada ya mapambano 20 na hakuna siri alizidiwa mno na Mbunge wa Ufilipino pamoja na kujitahidi kumaliza Raundi 12 kwa mateso.

    Mara ya mwisho, Pacquiao alimpiga Timothy Bradley wakati Algieri alimshinda Ruslan Provodnikov.
    Sasa, mjadala unaofuata ni Pacquiao kukutana na ulingoni na bondia ambaye hajawahi kupoteza pambano na mpinzani wake mkubwa, Floyd Mayweather Jr.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANNY PACQUIAO AMTWANGA CHRIS ALGIERI ALIYEKUWA HAJAPIGWA HATA MARA MOJA KABLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top