• HABARI MPYA

  Wednesday, November 19, 2014

  ZAMBIA WAPETA AFCON, MSUMBIJI WAISHIA ZIMPETO

  TIMU ya taifa ya Zambia imeifunga Cape Verde 1-0 na kulipa kisasi kizuri katika mbio za Mataifa ya Afrika 2015 mchezo wa Kundi F leo Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola hivyo kufuzu kwenye AFCON ya mwakani.
  Mchezo wa awali, Septemba 10 Cape Verde iliifunga Zambia 2-1 mjini na leo Chipolopolo imelipa kisasi kwa bao pekee la Ronald Kampamba dakika ya 77.
  Zambia inamaliza mechi za makundi ikiwa na pointi 11, moja zaidi ya Cape Verde wanayofuzu nayo AFCON. Msumbiji na Niger zilizotoka 1-1 leo, zote zimekwama kufuzu.
  Zambia wamefuzu vizuri AFCON baada ya ushindi wa 1-0 leo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZAMBIA WAPETA AFCON, MSUMBIJI WAISHIA ZIMPETO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top