• HABARI MPYA

  Wednesday, November 26, 2014

  KINDA YANGA ALIYETIMKIA ASIA AREJEA LEO OFA YA COASTAL INAMSUBIRI

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIUNGO chipukizi wa Yanga SC, Bakari Masoud aliyekuwa Malaysia kutafuta timu ya kuchezea, anatarajiwa kurejea leo Dar es Salaam.
  Bakari ‘Beka’ aliondoka jana Malasyia na leo anatarajiwa kufika Dar es Salaam, ingawa hatarejea tena Jangwani, kwa kuwa amemaliza Mkataba.
  Hata hivyo, bahati iliyoje kwake, klabu nyingine ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Coastal Union inamtaka ‘kwa udi na uvumba’.
  “Ninaondoka leo (jana) hapa na kesho (leo) nitakuwa Dar es Salaam. Ila sirudi Yanga, nikifika kwanza nitawasiliana na Coastal ambao wananihitaji,”amesema.
  Bakari Masoud 'Beka Mtaalamu' enzi zake Yanga SC


  Beka Mtaalamu ndani ya Malaysia

  Beka amesema sababu za kuondoka Yanga SC ni kutafuta nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza ili kukuza kiwango chake.
  “Yanga SC ni timu yangu, imeniibua na imenilea vizuri, nimekwenda Uturuki na Yanga, kwa kweli nina mengi ya kuwashukuru. Ila wakati umefika nitafute timu ambayo nitapata nafasi ya kucheza,”amesema.
  Akizungumzia kuhusu Malaysia, alisema kwamba alifanikiwa kufuzu majaribio katika timu ambayo inacheza Ligi Daraja la Tatu, lakini hakurudhika.
  “Maslahi hayakuwa mabaya, ila nilichokiona nahitaji changmoto zaidi kuliko kucheza Ligi Daraja la Tatu Malaysia. Kuna timu nyingine nilipata ya Daraja la Kwanza, lakini mazingira yake hayakuniridhisha,”amesema.  
  Bakari Masoud alikuwepo kwenye kikosi cha Yanga SC msimu uliopita na alikuwa miongoni mwa makinda ambao walikuwa wanamvutia kocha wa zamani wa timu hiyo, Mholanzi Ernie Brandts aliyemopandisha kutoka timu B. 
  Hata hivyo, alianza kukata tamaa baada ya ujio wa kocha mwingine, Mholanzi pia, Hans van der Pluijm na kuamua kwenda kujaribu bahati yake bara Asia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KINDA YANGA ALIYETIMKIA ASIA AREJEA LEO OFA YA COASTAL INAMSUBIRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top