• HABARI MPYA

  Tuesday, November 25, 2014

  SAAD KAWEMBA ‘ALIYENG’ARA’ TFF YA TENGA AWA MTENDAJI MKUU AZAM FC

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Saad Kawemba ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam.
  Kawemba ametambulishwa rasmi leo na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Sheikh Said Muhammad makao makuu ya klabu, Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  “Nafurahi kupata nafasi hii, ni fursa nyingine tena ya kupata uzoefu mwingine katika uongozi wa soka baada ya kufanya kazi kwa mafanikio TFF,”amesema Kawemba.
  Saad Kawemba kushoto amekuwa Mtendaji Mkuu wa Azam FC

  Bodi ya Ukurugenzi ya Azam FC imefikia hatua ya kuajiri Mtendaji Mkuu, ili kurahisisha uendeshaji ndani ya klabu kwa lengo la kutafuta ufanisi zaidi.
  Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba anatarajia kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wote wa klabu hiyo bingwa Tanzania Bara.
  Kawemba alifanya kazi TFF wakati wa Rais, Leodegar Chilla Tenga kabla ya kuondolewa baada ya kuingia uongozi mpya, chini ya Rais, Jamal Malinzi Oktoba mwaka jana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAAD KAWEMBA ‘ALIYENG’ARA’ TFF YA TENGA AWA MTENDAJI MKUU AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top