• HABARI MPYA

    Thursday, November 20, 2014

    ‘MCHEZAJI MPYA’ SIMBA ATAMBA TUZO ZA LIGI KUU KENYA, NA NDIYE KINARA WA MABAO KPL

    Na Vincent Malouda, NAIROBI
    MCHEZAJI anayetajwa kwenye orodha ya nyota wanaowaniwa na klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, Dan Sserunkuma usiku wa jana ameng’ara katika tuzo za Ligi Kuu ya Kenya zilizofanyika katika hoteli ya Safari Park mjini Nairobi.
    Kiungo wa Sofapaka Anthony Ekaliani Ndolo alijinyakulia mataji mawili makuu; ya mchezaji na kiungo bora wa mwaka huku kocha wake raia wa Uganda Sam Timbe akimaliza wa pili baada ya Mike Mururi wa Chemelil Sugar kwenye tuzo za kocha bora.
    Gor Mahia kwa upande wao walijivunia ushindi wa David Owino na Ronald Ngala kwenye safu ya beki bora na mwenyekiti bora mtawalia na kisha timu hiyo kuibuka ya pili kwenye timu yenye mchezo bora msimu huu. 
    Dan Sserunkuma mwaka jana alikuwa Mchezaji Bora wa Ligi ya Kenya
    Kiungo wa Gor na mganda Geoffrey ‘Baba’ Kizito naye alitangazwa nambari mbili kweny tuzo za kiungo na mchezaji bora huku mlindamlango Jerim Onyango akimaliza wa pili kwenye tuzo za kipa bora wa mwaka, nyuma ya Jairus Adira wa Chemelil Sugar.
    Kwenye tuzo zingine, Dan Sserunkuma mzawa wa Uganda alitwaa taji la daluga la mfungaji bora kwa kucheka na nyavu mara kumi na sita msimu huu, Hamisi Mwinyi wa Chemelil Sugar akizawidiwa mchezaji mwenye mchezo bora naye William Muluhya wa Mathare United akaibuka timu meneja bora mbele yake Amenipa Bigisho na George Maina wa Sofapaka na Thika United.
    Waamuzi wasimamizi wa mechi pia hawakuachwa nyuma kwani Peter Waweru na Steven Oduor walitangazwa refa na msaidizi wake bora mtawalia.
    Hafla hiyo ilihudhuriwa na rais wa Shirikisho la Soka la Kenya Sam Nyamweya na mwenyekiti wa ligi kuu Ambrose Rachier miongoni mwa viongozi wengine.
    Dan Sserunkuma akimtoka mchezaji wa KCCA ya Uganda katika Kombe la Kagame mwaka huu mjini Kigali, Rwanda

    TUZO ZA WACHEZAJI NA MAKOCHA/VIONGOZI BORA MWAKA 2014
    Mchezaji Bora: Ekaliani Ndolo (Sofapaka)
    Kipa Bora: Jairus Adira (Chemelil Sugar)
    Beki Bora: David Owino (Gor Mahia)
    Kiungo Bora: Ekaliani Ndolo (Sofapaka)
    Daluga la Mfungaji Bora: Dan Sserunkuma (Gor Mahia)
    Mchezo Bora: Hamisi Mwinyi (Chemelil Sugar)
    Timu yenye Mchezo Bora: Muhoroni Youth
    Kocha Bora: Mike Mururi (Chemelil Sugar)
    Timu Meneja Bora: William Muluhya (Mathare United)
    Mwamuzi Bora: Peter Waweru
    Naibu Muamuzi Bora: Steven Oduor
    Mwenyekiti Bora: Ronald Ngala (Gor Mahia)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ‘MCHEZAJI MPYA’ SIMBA ATAMBA TUZO ZA LIGI KUU KENYA, NA NDIYE KINARA WA MABAO KPL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top