Na Vincent Malouda, NAIROBI
HUENDA ligi kuu ya taifa la Kenya ikawa na jumla ya timu kumi na nane kwanzia msimu ujao wa 2015 iwapo pendekezo la Shirikisho la Soka la Kenya, FKF, la kupandisha timu mbili zaidi kutoka daraja la pili likafua dafu.
Kamati ya utendaji ya Shirikisho hilo imetoa mapendekezo matatu makuu ili kuafikia swala hilo;
La kwanza ni kwamba timu itakayoburura manyoya ndio itakayoshushwa daraja, Top Fry AllStars wakijipata kwenye mtego huo baada ya kumaliza nafasi ya mwisho msimu uliyopita uliyotamatika wikendi iliyopita.
Pili ni kuwa washindi wa Zoni A na B kwenye ligi ya darala la pili yenye timu kumi na mbili kila upande ndiyo watakaofuzu ligi kuu ya taifa huku wanaomaliza nambari mbili wakimenyana kwenye mechi ya muondoano ambapo mshindi atajikatia tiketi ya kushiriki ligi kuu, hilo likiwa pendekezo la tatu.
Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano John Kariuki alimaarufu ‘FIFA’, Posta Rangers FC na Shabana FC tayari wamefuzu ligi kuu baada ya kuongoza jedwali la ligi ya daraja la pili Zone A na B katika usanjari huo japo zipo tetesi kuwa Shabana FC wamerejea katika ligi kuu ya taifa kwa kutumia mlango wa nyuma hasa baada ya kutunikiwa alama 12 za bwerere. Ibainike kuwa mlezi wao ni vile vile rais wa shirikisho Sam Nyamweya.
Kwa mujibu wa pendekezo la tatu, Nakumatt FC (Zoni A) na Kakamega Homeboyz (Zoni B) watakabiliana kwenye mechi ya muondoano tarehe 22 Novemba mjini Nakuru, mshindi akijiunga nao Posta na Shabana kujumuisha timu kumi na tano za ligi hadi kumi na nane kabla ya msimu ujao.
Kwenye mfumo wa sasa, timu mbili za mwisho ndizo zinazopigwa shoka kwa maana ya Nairobi City Stars na Top Fry AllStars lakini iwapo pendekezo hilo litazaa matunda basi Nairobi City Stars wataliepuka shoka.
Swala hilo hata hivyo lazima liungwe mkono na kamati ya utendaji ya ligi kuu ya taifa na wafadhili wakuu SuperSport kwa maelewano zaidi. Gor Mahia ndio mabingwa watetezi wa msimu wa 2014.

0 comments:
Post a Comment