• HABARI MPYA

  Thursday, November 27, 2014

  LIVERPOOL YABANWA, SARE 2-2 ULAYA

  LIVERPOOL imelazimishwa sare ya 2-2 na Ludogorets katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu.
  Wenyeji, Ludogorets walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Dani Abalo dakika ya tatau, kabla ya Liverpool kusawazisha kupitia kwa Rickie Lambert dakika ya nane.
  Wekundu wa Anfield walipata nao lililoelekea kuwa la ushindi kupiti kwa Jordan Henderson dakika ya 37 kabla ya Georgi Terziev kuisawazishia Ludogorets dakika ya 88.
  Kikosi cha Ludogorets kilikuwa; Stoyanov, Junior Caicara, Moti, Terziev, Minev, Misidjan, Dyakov, Fabio Espinho/Younes dk80, Mihail Aleksandrov/Wanderson dk72, Marcelinho na Dani Abalo/Quixada dk69.
  Liverpool: Mignolet, Johnson, Skrtel, Toure, Manquillo, Henderson, Gerrard, Lucas, Lambert, Allen na Sterling/Moreno dk82.
  Liverpool's Steven Gerrard and Rickie Lambert look dejected after George Terziev (not pictured) scored for Ludogorets
  Wachezaji wa Liverpool, Steven Gerrard na Rickie Lambert wakiwa wanyonge baada ya George Terziev (hayupo pichani) kuisawazishia Ludogorets

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2850777/Ludogorets-2-2-Liverpool-Late-Georgi-Terziev-goal-rescues-point-Bulgarians-Brendan-Rodgers-hopes-16-place-jeopardy.html#ixzz3KDWNmEsA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YABANWA, SARE 2-2 ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top