• HABARI MPYA

  Sunday, November 30, 2014

  KIPA YANGA SC APATA DHORUBA HADI KUPOTEZA FAHAMU UARABUNI

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIPA wa zamani wa Yanga SC, Juma Mpongo jana ‘amechungulia kifo’ baada ya kupigwa na daluga la mchezaji mwenzake uwanjani kiasi cha kuzimia kwa zaidi ya saa nne.
  Mpongo anayedakia Seeb ya Muscat, Oman alizimia jana dakika ya 70 katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Boshar na kukimbizwa hospitali ya Badri Alsamaa.
  Katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana, Mpongo anasema aliumia wakati anaruka juu kudaka krosi ya wapinzani wao.
  “Kwa kweli sikujua nini kimetokea, ila jana kocha wangu Spear Mbwembwe ndiyo kanielezea kuwa niliruka juu kudaka krosi, wachezaji kama watatu wa Boshar wakanivamia. Ndivyo ilivyokuwa,”amesema Mpongo akizungumza na BIN ZUBEIRY kwa simu kutoka Oman leo.
  Juma Mpongo akiwa hospitali baada ya kuumia jana
  Mpongo akionyesha sehemu ambayo aligongwa jana

  Kipa huyo aliyewahi pia kudakia Coastal Union ya Tanga, amesema kabla ya juzi, wiki moja iliyopita pia aliumia tena wakicheza na Boshar pia kwenye michuano ya Kombe la Mazda. 
  “Nilidaka mpira na mshambuliaji alikuwa anapiga, akapiga upande wa kushoto kwenye ini, lakini nashukuru ini halikupata matatizo, baada ya saa kama nne hivi ya vipimo na uchunguzi, ikagundulika nipo sawa,”amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPA YANGA SC APATA DHORUBA HADI KUPOTEZA FAHAMU UARABUNI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top