KLABU ya Barcelona imethibitisha mchezaji wao majeruhi, Thomas Vermaelen atafanyiwa upasuaji na daktari wa Finland, Sakari Orava Jumanne ijayo na atakuwa nje kwa miezi minne hadi mitano.
Orava, mpasuaji aliyejipatia umaarufu baada ya kumfanyia huduma hiyo Jonathan Woodgate alipokuwa majeruhi kiasi cha kuchelewa kuanza kazi Real Madrid, sasa atamtimu Vermaelen, mwenye umri wa miaka 29, ambaye ameambiwa anahitaji upasuaji kuokoa soka yake.
Beki huyo wa zamani wa Arsenal aliumia akiwa kwenye kikosi cha timu yake ya taifa, Ubelgiji wakati wa mechi dhidi ya Urusi Kombe la Dunia miezi mitano iliyopita, lakini wakati Barcelona inamsajili Mkurugenzi wa Michezo Andoni Zubizarreta alisema alikuwa ‘tayari kwa kazi’.
0 comments:
Post a Comment