• HABARI MPYA

  Friday, November 28, 2014

  CECAFA: HATUJALALA, TUNAHANGAIKA CHALLENGE IFANYIKE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limesema bado linahangaikia kufanyika kwa michuano ya Kombe la Challenge mwaka huu.
  Meneja wa Vyombo vya Habari wa CECAFA, Rogers Mulindwa amesema leo kwamba,  michuano ya Challenge ambayo awali ilikuwa ifanyike Ethiopia, lakini ikajivua uenyeji, bado ipo kwenye uwezekano wa kufanyika.
  “Kamati Kuu ya CECAFA chini ya Mwenyekiti, Mhandisi Leodgar Tenga na Katibu Mkuu, Nicholas Musonye bado inafanyia kazi uwezekano wa kuhakikisha michuano hiyo inafanyika mwaka huu,” amesema Mulindwa.
  Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye anahangaikia Challenge ifanyike
  Mganda huyo amesema kwamba  CECAFA baadaye itatoa taarifa rasmi juu ya mustakabali wa mashindano ambayo hufanyika mwishoni mwa Novemba hadi mwanzoni mwa Desemba.
  Nchi wanachama wa CECAFA ni Sudan, Ethiopia, Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, Somalia, Eritrea, Djibouti, Zanzibar na Sudan Kusini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CECAFA: HATUJALALA, TUNAHANGAIKA CHALLENGE IFANYIKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top