• HABARI MPYA

  Tuesday, November 25, 2014

  AZAM FC YASEMA MKALI WA MABAO TRAORE ANAKUJA CHAMAZI, KOCHA OMOG KUAMUA HATIMA YA KIEMBA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imesema kwamba imefikia kwenye hatua nzuri ya mpango wa kumleta mshambuliaji wa kimataifa wa Mali, Mohamed Traore.
  Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, wamefikia pazuri katika mazungumzo na klabu ya Traore, El Merreikh ya Sudan.
  “Nadhani kufikia mwishoni mwa wiki tutakuwa na cha kuzungumza kuhusu Traore,”amesema.
  Kuhusu beki Said Mourad ambaye Mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu, Kawemba amesema mazungumzo na mchezaji huyo yanaendelea ili aongeze Mkataba.
  Mohamed Traore anakuja Azam FC

  Kuhusu kiungo Amri Kiemba, Kawemba amesema mchezaji huyo amewasili Azam FC kwa mkopo kumalizia Mkataba wake wa klabu yake, Simba SC ambao unatarajiwa kufikia tamati Juni 15, mwakani.
  “Baada ya kumalizia Mkataba wake wa Simba SC, sasa mwalimu (Joseph Marius Omog) ataamua hatima ya Kiemba, kama apewe Mkataba mpya na klabu yetu, au la” ameongeza Kawemba.
  Aidha, Kawemba amesema kwamba kocha Msaidizi, Mganda George ‘Best’ Nsimbe anatarajiwa kuwasili mwishoni mwa wiki kuja kuanza kazi.
  “Nsimbe tulikwishasaini naye Mkataba, alikuwa anamalizana na klabu yake KCCA, kwa hiyo mwishoni mwa wiki atakuwa tayari ameripoti kazini,”amesema Kawemba. 
  Nsimbe anakuja kuchukua nafasi ya Muingereza Kali Ongala, aliyejiuzulu mapema mwezi huu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YASEMA MKALI WA MABAO TRAORE ANAKUJA CHAMAZI, KOCHA OMOG KUAMUA HATIMA YA KIEMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top