• HABARI MPYA

  Sunday, November 30, 2014

  BENO NJOVU ‘OUT’ YANGA SC, PANGA LA MANJI LAWAWINDA WENGINE ZAIDI

  Na Abdul Salim, DAR ES SALAAM
  MKATABA wa Katibu wa Yanga SC, Benno Njovu unamalizika leo na kwa bahati mbaya klabu hiyo haina mpango naye tena.
  Habari kutoka ndani ya klabu hiyo, zimesema kwamba Njovu ni mtu safi, lakini uongozi umebaini masuala ya soka ‘yanampiga chenga’ kidogo, hivyo wanahitaji mtu mwingine katika nafasi hiyo.
  Habari zaidi zinasema kwamba, tayari Njovu amekwishafungasha kila kilicho chake kutoka katika ofisi aliyorithi kwa Lawrence Mwalusako, beki wa zamani wa Yanga SC.
  Benno Njovu amemaliza Mkataba Yanga SC na klabu hiyo haina haja naye tena 
  Bado haijulikani nani atarithi nafasi ya Njovu, lakini BIN ZUBEIRY inafahamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji atafanya mabadiliko zaidi katika Sekretarieti ili kutafuta ufanisi.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BENO NJOVU ‘OUT’ YANGA SC, PANGA LA MANJI LAWAWINDA WENGINE ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top