• HABARI MPYA

  Tuesday, November 25, 2014

  PELE AREJESHWA HOSPITALI

  GWIJI wa soka Brazil, Pele amerejeshwa hospitali jana mjini Sao Paulo, siku kadhaa baada ya kufanyiwa upasuaji wa figo.
  "Mpendwa wetu Edson Arantes do Nascimento (Pele) amerejeshwa kwa matibabu zaidi na anaendelea vizuri," imesema taarifa ya hospitali ya Albert Einstein.
  Vyombo vya Habari nchini Brazil viliripoti kwamba Pele alikuwa anatibiwa kwa maradhi ya mkojo.
  Pele anasumbuliwa na matatizo ya Kiafya na jana amerejeshwa hospitalia kwa matibabu

  Pele, mwenye umri wa miaka 74 sasa,alikwenda kufanyiwa upasuaji Novemba 13 akisumbuliwa na mawe ya figo.
  Jamaa wa karibu, Jose Fornos Rodrigues ameliambia Shirika la Habari Ufaransa, AFP Pele angelazwa hospitali ya Einstein Hospital, lakini hakuzama ndani zaidi.
  Pele, alizaliwa katika jamii ya watu wanyenyekevu kwenye mii wa Tres Coracoes, kabla ya kuwa gwiji wa soka aliyeheshimika ulimwengu mzima.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PELE AREJESHWA HOSPITALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top