• HABARI MPYA

  Thursday, November 20, 2014

  LIGI DARAJA LA PILI SASA KUANZA KUTIMUA VUMBI DESEMBA 6

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  LIGI Daraja la Pili (SDL) msimu huu iliyokuwa ianze kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu kwa mechi kumi katika viwanja vitano tofauti imesogezwa mbele hadi Desemba 6 mwaka huu.
  Mechi hizo zimesogezwa ili kutoa fursa ya kukamilisha maandalizi mbalimbali ya ligi hiyo inayoshirikisha timu 24 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.
  Mikoa yenye timu katika ligi hiyo ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Katavi, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe, Pwani, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Singida na Tabora.
  CDA ya Dodoma pia itashiriki Ligi Daraja la Pili
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIGI DARAJA LA PILI SASA KUANZA KUTIMUA VUMBI DESEMBA 6 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top