• HABARI MPYA

  Saturday, November 22, 2014

  MAN UNITED 'WAJILIA RAHA' KWA ARSENAL, WAWACHAPA 2-1 EMIRATES

  MANCHESTER United imeendeleza ubabe dhidi ya Arenal, baada ya usiku huu kuichapa mabao 2-1 Uwanja wa Emirates katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. 
  United walipata bao la kwanza dakika ya 56, baada ya beki Kieran Gibbs kumfunga mwenyewe kipa wake, Wojciech Szczesny katika harakati za kuokoa krosi ya Antonio Valencia, kabla ya Nahodha Wayne Rooney kufunga la pili dakika ya 85 akimalizia pasi ya Angel di Maria. Olivier Giroud aliifungia Arsenal la kufutia machozi dakika ya 90.
  Beki wa United, Luke Shaw alitolewa nje dakika ya 16 baada ya kuumia kifundo cha mguu, wakati kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere alinusurika kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Marouane Fellaini.
  Lakini kiungo huyo wa England alitolewa nje dakika ya 55 baada ya kuumia pia.  Kipa Szczesny pia alitolewa uwanjani baada ya kuumia.
  Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny/Martinez dk59, Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Ramsey/Giroud dk77, Arteta, Wilshere/Cazorla dk55, Oxlade-Chamberlain, Welbeck na Sanchez
  Manchester United; De Gea, Smalling, McNair, Blackett, Valencia, Carrick, Fellaini, Di Maria, Shaw/Young dk16/Fletcher dk89, Rooney na Van Persie/James Wilson dk75.
  Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney (kulia) akishangilia baada ya Kieran Gibbs kujifunga 

  Woljciech Szczesny na Kieran Gibbs wa Arsenal wakipamiana kabla ya kujifunga

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2837001/Arsenal-vs-Manchester-United-Team-news-kick-time-probable-line-ups-odds-stats-Premier-League-clash.html#ixzz3JpEIaEU5
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED 'WAJILIA RAHA' KWA ARSENAL, WAWACHAPA 2-1 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top